Couverture de Neno la Leo

Neno la Leo

Neno la Leo

De : Neno la Leo 255
Écouter gratuitement

Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.

Neno la Leo 255
Christianisme Ministère et évangélisme Spiritualité
Épisodes
  • Kwa Nini Mungu Huacha Utaabike? Nini cha Kufanya?
    Jul 1 2026

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

    Leo tunatafakari Waamuzi 10:6–8 na 10:15–16. Waisraeli walipoanza kumwacha Mungu na kufuata miungu mingine, walivuna matokeo ya maamuzi yao. Lakini walipomrudia kwa toba ya kweli na kuacha kabisa yale yaliyowatenga naye, Mungu aliwaonyesha rehema na huruma zake. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba kuondoka kwa Mungu kuna gharama, lakini kurudi kwake kwa moyo wa kweli daima hufungua mlango wa neema na urejesho. Je, kuna eneo katika maisha yako ambalo Mungu anakualika urudi kwake leo?

    Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

    Afficher plus Afficher moins
    25 min
  • Je, Imani Yako Ni Yako Kweli? Au Umeazima?
    Jun 30 2026

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

    Leo tunatafakari Waamuzi 8:33–34. Baada ya kifo cha Gideoni, Waisraeli walimsahau Mungu na kurudia njia zao za zamani. Kupitia simulizi hili tunajifunza kwamba imani ya kweli haiwezi kutegemea mtu mwingine bali inapaswa kujengwa katika uhusiano binafsi na Mungu. Pia tunakumbushwa kwamba mara nyingi kuanguka huanza pale tunaposahau fadhili na matendo makuu ambayo Mungu ametutendea.

    Karibu tusikilize, tutafakari na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. 🙏📖✨

    Afficher plus Afficher moins
    25 min
  • Pale Tunapobaki na Mungu Peke Yake!
    Jun 29 2026

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo

    Leo tunatafakari simulizi ya Gideoni na jeshi la watu 300 kutoka Waamuzi 7:1–8. Mungu alipunguza jeshi la Israeli ili ushindi usihesabiwe kuwa ni matokeo ya nguvu za wanadamu bali ya uwezo wake. Kupitia somo hili tunajifunza kwamba wakati mwingine Mungu hupunguza kile tunachokitegemea ili kutufundisha kumtegemea Yeye zaidi. Je, inawezekana kwamba kile unachokiona kama upungufu ni maandalizi ya Mungu kwa ushindi mkubwa zaidi?

    Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

    Afficher plus Afficher moins
    12 min
adbl_web_anon_alc_button_suppression_t1
Aucun commentaire pour le moment